Jumatano 11 Februari 2026 - 02:00
Waislamu wa Kanada waupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuwasha taa na kuweka mapambo mitaani

Hawza/ Mwezi wa Ramadhani, ambao ndani ya British Columbia unajulikana kama Sherehe ya Ramadhani, mwaka huu unaangukia mwishoni mwa Februari na mwanzoni mwa mwezi Machi. Katika mji wa Surrey, sherehe ya siku nne pamoja na futari kwa wananchi imeandaliwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, baada ya msafara wa sherehe ya Ramadhani mwaka uliopita kufanyika kwa mafanikio makubwa na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 50,000, mwaka huu pia sherehe hiyo imepangwa kufanyika kwa siku nne mfululizo, huku ikiambatana na futari na aina mbalimbali za mapokezi.

Aidha, mji wa Surrey kila majira ya joto huwa mwenyeji wa tamasha kubwa la chakula cha halali, linalowakusanya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za Kanada.

Waandaaji wametoa maelezo kuhusu namna sherehe hiyo itakavyofanyika: tukio hilo litadumu kwa siku nne, likiwa na zaidi ya vibanda 100 vya vyakula vya halali, pamoja na programu mbalimbali za kuvutia zikiwemo mapambo ya taa yaliyoandikwa Ramadhani, vipindi vya moja kwa moja na swala ya jamaa.

Chanzo: About Islam

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha